Drake Alivyonunua Nyumba Ya Jirani Kisa Kelele

Drake Alivyonunua Nyumba Ya Jirani Kisa Kelele

Rapa na mwanamuziki maarufu kutoka Canada, Drake ambaye anajulikana kwa maisha yake ya kifahari na mapenzi makubwa katika muziki, inaelezwa kuwa aliwahi kununua nyumba ya jirani yake baada ya jirani huyo kulalamika kupigiwa kelele.

Mwaka 2016 Drake alinunua nyumba ya jirani yake kwa dola milioni 2.85 ikiwa ni zaidi ya Sh 7.5 bilioni baada ya kushitakiwa na jirani yake ambaye alidai kuwa msanii huyo alikuwa akifungulia muziki kwa sauti ya juu jambo ambalo lilikuwa kero kwake.

Hata hivyo baada ya Drake kupata malalamiko hayo ndipo akajiwekea sheria ya kununua nyumba ya jirani yoyote atakayelalamika kuhusu kelele zake ili aweze kuwa huru.

Mbali na tukio hilo kuwashangaza wengi tukio jingine lililowaacha mashabiki hoi ni la mwaka 2022 ambapo alikodi mgahawa mzima wa Dodger Stadium uliopo jijini Los Angeles kwa ajili ya mazungumzo na aliyekuwa mpenzi wake Johanna Leia.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags