Rapa wa Marekani mwenye asili ya Canada, Drake ameripotiwa kufuta kesi aliyoifungua dhidi ya Spotify na Universal Music Group baada ya kuzishutumu taasisi hizo kwa kuanzisha mpango usio halali wa kuongeza namba ya wasikilizaji ili kuupa umaarufu wimbo wa "Not Like Us" wa Kendrick Lamar.
Kwa mujibu wa jarida la 'Variety' ambao walizinyaka Hati ya kesi hiyo kutoka mahakamani inaeleza kuwa Drake alikutana na wawakilishi wa Spotify na UMG siku ya Jumanne, Januari 14, 2025, na kufikia makubaliano ya kuondoa kesi hiyo bila gharama kwa pande yoyote.
Kesi hiyo ilipangwa kuanza kusikilizwa Januari 28, 2025 ambapo Drake alizifungulia mashtaka kampuni za Universal Music Group pamoja na Spotify Mwezi Novemba, 2024 akidai kwamba wametumia njia isiyo sahihi kwa kutengeneza namba (streams) nyingi za wimbo wa Kendrick Lamar ‘Not Like Us’ ambao uliachiwa Mei 4, 2024.
Drake kupitia kampuni yake ya Frozen Moments LLC, alizishtaki kampuni hizo akidai wametumia maroboti na mifumo mingine ya udanganyifu kuupaisha kinamba na usikilizwaji wimbo wa hasimu wake huyo.
Hata hivyo Universal Music Group walitoka hadharani na kupinga madai hayo ambapo wamesema hakuna kitu kama hicho kwani kila msanii anapata anachostahili kimkataba na hakuna njia za udanganyifu
Leave a Reply