Don afunguka kuhusu afya ya Professor Jay

Don afunguka kuhusu afya ya Professor Jay

Moja kati ya story ambayo ni gumzo katika mitandao ya kijamii ni kuumwa kwa msanii wa Hip hop, Joseph Haule maarufu kama  Professor  Jay ambapo mambo mengi yamezungumzwa lakini sisi tumekusogezea ripoti iliyotolewa na mtu wa karibu wa msanii huyo.

Don Colean255 ni mtu wa karibu na Professor Jay ambaye amesema hali ya msanii huyo bado si nzuri na kwa sasa yupo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akiendelea na matibabu.

Rafiki huyo alisema tangu Jumatatu ya Februari 24, mwaka huu Professor Jay hali yake ilibadilika na kupelekwa hospitali ya Lugalo ambayo baada ya kumpima walimuhamishia Muhimbili kutokana na hali yake kutokuwa nzuri.

“Kwa hiyo mpaka sasa tupo Muhimbili na hali yake bado haijatengamaa kwa sababu hata madaktari bado hawajatupatia mrejesho wowote mpaka sasa,” alisema.

Endelea kutufatilia tutakujuza kila kinachoendelea






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags