DOGO JANJA: SITOSIKIKA SANA MWAKA HUU

DOGO JANJA: SITOSIKIKA SANA MWAKA HUU

Msanii  Dogo Janja unaambiwa amefunguka tunaweza kusema hivyo kutokana na  kusapoti wasanii wapya kwa 2022 ikiwa ni kama kurudisha  kwa jamaii ambapo amesema kuwa ni muda wakuwapa wasanii wapya nafasi.

Kupitia mahojiano na kituo kimoja cha habari amesema “Katika maisha yangu ya muziki nadhani historia yangu ya mimi kutoka kila mtu anaijua so nadhani pia huu ni muda wa mimi kurudisha katika jamii, mwaka huu sitarajii kufanya mimi sana lakini nitakuwepo nyuma ya huu muziki, kwahiyo nadhani ni muda wakuwapa nafasi watu wapya wenye vipaji" Dogo janja.

"Tunaweza kuwaombea masikio kwasababu tunaamini wakisikika watazingatiwa, hata Madee huwa namwambia kuwa natamani na mimi siku moja nirudishe katika jamii so huu umekuwa ni muda mzuri sana na uzuri kuna baraka kwa mabraza hivyo ni kitu kizuri sana" Dogo janja.

Haya sasa kwa maoni yako mdau unaweza kushare nasi kupitia ukurasa wetu wa instagram pia ukatoa mtazamo wako juu ya suala hilo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags