Ikiwa imepita miezi sita sasa tangu mwili wa marehemu mwanamuziki wa Nigeria, Mohbad kufukuliwa, sasa imeripotiwa kuwa matokeo ya uchunguzi wa maiti hiyo yatakuwa tayari wiki nne zijazo.
Maelezo hayo yametolewa na Dkt Richard Somiari, Mkurugenzi wa Kituo cha DNA na Uchunguzi Jimbo la Lagos, wiki hii ambapo alieleza kuwa matokeo ya uchunguzi wa mwili wa Mohbad yanatarajiwa kutangazwa wiki tatu au nne zijazo, huku akiuhakikishia umma kuwa usalama wa sampuli hizo ni mathubuti.
Mwanamuziki Mohbad (27) alifariki Septemba 12, 2023, huku kifo chake kikizua utata na kusababisha Serikali Jimbo la Lagos kufanya uchunguzi wa kifo hicho ambapo uchunguzi huo ulianza rasmi Oktoba 13, 2023, katika Mahakama ya Mwanzo ya Ikorodu.
Hata hivyo kutokana na kifo cha Mohbad baadhi ya watu kama vile Naira Marley, Sam Larry na Prime walituhumiwa kwa kifo hicho.
Leave a Reply