Diva, Niffer Kuhojiwa Na Polisi Dar

Diva, Niffer Kuhojiwa Na Polisi Dar

Jeshi la Polisi linawashikilia kwa mahojiano ya kina Diva Malinzi (36) na Jenifer Jovin (25) maarufu Niffer kwa tuhuma za kuchangisha fedha kwa ajili ya walioporomokewa na ghorofa eneo la Kariakoo.

Hayo yamebainishwa leo Jumanne Novemba 19, 2024 katika taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro.

“Watuhumiwa wawili wamekamatwa na wanahojiwa kwa kina. Waliokamatwa ni Diva Gissele Malinzi miaka 36, mkazi wa Mikocheni amekamatwa Dar es Salaam na Jenifer Jovin miaka 25, mkazi wa Salasala Kinondoni ambaye amekamatwa Dodoma na kurejeshwa Dar as Salaam,” inaeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Jeshi la Polisi litashirikiana na mamlaka zingine za kisheria kuona hatua zinazopaswa kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa hao.

Jengo hilo liliporomoka Jumamosi Novemba 16, 2024 na kusababisha vifo vya watu 16 na wengine zaidi ya 80 kujeruhiwa.

Endelea kufuatilia Mwananchi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags