Diddy mbioni kufunguliwa kesi ya jinai

Diddy mbioni kufunguliwa kesi ya jinai

‘Rapa’ Sean “Diddy” Combs huenda akafunguliwa kesi ya jinai na mwanadada Adria English. Kwa mujibu wa timu ya wanasheria wa mwanadada huyo imedai kuwa English yupo mbioni kufungua kesi kwa ajili ya kudai fidia ya dola 50 milioni kutoka kwa Diddy kufuatia kulazimishwa kutumia kiasi kikubwa cha pombe na kufanyiwa vitendo visivyofaa bila idhini yake.

Utakumbuka kuwa mwanadada huyo aliwahi kuwasilisha kesi dhidi ya Diddy Julai mwaka huu akidai alilazimishwa kushiriki katika biashara ya ngono mwaka 2004-2009 wakati alipokwenda kwenye sherehe za Combs alizokuwa akizifanya nyumbani kwake New York na Miami.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na timu ya wanasheria wa English imeweka wazi kuwa mwanadada huyo ameamua kurudi tena mahakamani kwa ajili ya kutaka haki kama ilivyo kwa watu wengine ambao tayari wamewasilisha kesi mahakamani.

“English anafuraha sana na matumaini kuhusu safari yake ya kutafuta haki, kuanzia kufungua kesi ya madai Julai 3, 2024, English anatarajia kufungua malalamiko ya ziada ya jinai huko New York lakini amezuiliwa kwa sasa kwa kuwa New York inahitaji mlalamikaji kwenda kufungua kesi mwenyewe na siyo kutuma wanasheria,” ameeleza mwanasheria wa English

Diddy amekuwa akiandamwa na kesi nane za unyanyasaji wa kingono lakini mpaka kufikia sasa bado hakujapatikana ushahidi madhubuti wa kumtia nguvuni huku baadhi ya mastaa wakidai kuwa Diddy ni FBA hivyo hatoweza kukamatwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags