Diddy Awavuruga Mashabiki

Diddy Awavuruga Mashabiki

Mwanamuziki na mfanyabiashara maarufu kutoka Marekani, Sean "Diddy" Combs, ameacha mashabiki wake wakiwa na maswali hii ni baada ya kuposti emoji ya kukodoa macho (👀) kwenye mtandao wa X (zamani Twitter) kisha kuifuta.



Emoji hiyo imekuja wakati ambao Diddy yupo gerezani kufuatia makosa mawili likiwemo la kuhusika na biashara ya ukahaba.

Baada ya kuposti na kufuta emoji hiyo, mashabiki wamezua mijadala katika mitandao ya kijamii ambapo baadhi yao wakiandika “Huyu jamaa ana jaribu kutuchokoza,” huku wengine wakisema, “Anaonekana bado ana ‘control’ ya attention ya watu.”

Sean "Diddy" Combs alikamatwa Septemba 16, 2024 katika hoteli ya Park Hyatt, Manhattan, New York na kupelekwa moja kwa moja katika gereza la Metropolitan. Kesi yake ilianza kusikilizwa Mei 5,2025 huku watu mbalimbali wakitoa ushahidi akiwemo mpenzi wake wa muda mrefu Cassie Ventura, Jane, Mia, Kid Cudi, Bongolani, mama mzazi wa Cassie na wengineo.

Hata hivyo hukumu ya kesi hiyo inatarajiwa kusomwa Oktoba 3,2025, huku Serikali inataka Combs ahukumiwe kifungo cha kati ya miezi 51 hadi 63 jela, lakini kwa upande wa utetezi unapendekeza kifungo kifupi cha kati ya miezi 21 hadi 27, aidha kuna uwezekano atapunguziwa kifungo kutokana na muda aliokaa jela kwa zaidi yam waka mmoja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags