Utafiti: Wanandoa Wanaokumbatiana Wakati Wa Kulala Wanafuraha

Utafiti: Wanandoa Wanaokumbatiana Wakati Wa Kulala Wanafuraha

Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na Josh R. Novak na mwanasaikolojia Kaleigh C. Miller kutoka chuo Chuo Kikuu cha Auburn, Marekani umebaini kuwa wanandoa wanaokumbatiana na kulala karibu usiku wanafuraha na mahusiano yao.

Utafiti huo ambao umewahusisha wanandoa 143 waliyo kwenye ndoa kwa takribani miaka 13na kugundua kuwa staili za kulala na mweza wao zinaweza kuboresha mahusiano na maelewano ya wanandoa.

Takwimu zilionesha kuwa asilimia 94 ya wanandoa wanaolala huku wamekumbatiana usiku waliripoti kuwa na mahusiano yenye furaha, huku asilimia 68 ya wanaolala mbalimbali wakiwa hawana furaha.

Aidha, lakini pia kwa wanandoa wanaolala karibu zaidi wakitazamana uso kwa uso wana uwezo wa kupungumza msongo wa mawazo na kuimarisha usalama wa mihemko katika uhusiano.

Hata hivyo, watafiti walibaini kuwa ingawa utafiti ulikuwa wa muda mfupi, lakini unaweza kuwa msingi mzuri wa kujua kuwa ukaribu wa kimwili wakati wa usiku kwa wanandoa unaboresha ustawi wa mahusiano pamoja na afya ya akili.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags