Diddy Akubali Kubaki Gerezani

Diddy Akubali Kubaki Gerezani

Baada ya kuomba dhamana kwa takribani mara tatu bila mafanikio, hatimaye msanii wa Hip Hop Marekani Diddy Combs amekubali kubaki gerezani hadi pale kesi yake itakapoanza kusikilizwa mwezi Mei 2025.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘Hollywood Unlocked’ wanasheria wa Combs wamewasilisha ombi la kufuta rufaa ya dhamana leo Desemba 14, 2024 katika mahakama iliyopo jijini New York.

“Kulingana na ombi hilo, Bw. Combs hatotaka kukata rufaa dhidi ya mahakama ya wilaya kwa kukataa ombi lake la dhamana lililofanywa upya, na kwa hivyo anaomba kufuta rufaa hiyo kwa hiari,” ameseama wakili wa Diddy

Combs alikamatwa kwa mara ya kwanza Septemba 16, 2024 jijini New York katika moja ya hoteli iliyopo jijini humo, ambapo kabla ya kukamatwa nyumba zake zilipigwa msako na kukutwa na mafuta zaidi ya chupa 1000.

Kwa sasa anazuiliwa katika gereza la ‘Metropolitan Detention’ huko Brooklyn, kwa makosa ya unyanyasaji wa ngono, usafirishaji haramu wa watu huku kesi yake ikianza kusikilizwa Mei 5, 2025.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags