Diamond na Rekodi mpya

Diamond na Rekodi mpya

Mwanamuziki wa Bongo Flava nchini, Diamond Platnumz, ameendelea kuonesha ukubwa wake baada ya kufikisha zaidi ya streams milioni 400 kwenye mtandao wa kuskiliza mziki wa ‘Boomplay Music’.

Hii ni rekodi nyingine kwa msanii huyo kufikisha streams hao na kumfanya kuandika historia mpya ya kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika Mashariki kufikia hatua hiyo kwa mara nyingine, kwani yeye ndio wa kwanza kufikia stream 100, 200, 300 na sasa ni 400.

Mbali na Diamond kuongoza katika ‘Golden club’ hiyo ya stream za boom play wapo baadhi ya wasanii ambao wanakaribia kufikia rekodi hiyo akiwemo Zuchu (300), Rayvanny (300), Mbasso (200), Jaymelody (200), Nandy (100), Alikiba (100) na wengineo.

Aidha anayeongoza rekodi hiyo barani Afrika ni mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria ambaye ameripotiwa kufikisha zaidi ya stream bilioni moja.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags