Diamond agonga mwamba tena Tuzo za Grammy

Diamond agonga mwamba tena Tuzo za Grammy

Licha ya ngoma ya ‘Komasava’ kufanya vizuri duniani kote lakini msanii Diamond Platnumz amegonga mwamba dhidi ya mastaa kutoka Nigeria katika kuwania tuzo za Grammy.


Utakumbuka mapema mwenzi Octoba Diamond aliwasilisha wimbo huo wenye zaidi ya watazamaji milioni 27 kwenye mtandao wa YouTube katika kinyang’anyiro cha Grammy lakini mambo yamekuwa magumu upande wake kwa jina lake kutotajwa kuwania tuzo hizo katika vipengele alivyoorodhesha.

Katika majina ya wasanii wanaowania tuzo yaliyotajwa na Grammy leo Octoba 8,mastaa kutoka Nigeria wameendelea kuzitawala tuzo hizo kwa kutajwa kwenye vipengele mbali mbali wakiwemo Yemi Alade - Tomorrow, Asake & Wizkid - MMS, Chris Brown Ft Davido - Sensational, Burna Boy - Higher na Tems - Love Me Jeje

Huku staa aliyeongoza kwa kutajwa mara nyingi katika tuzo hizo kwa ni Beyonce ambaye ameorodheshwa katika vipengele 11, kwa mujibu wa tovuti ya Billboard.

Diamond aliwasilisha majina yake kupitia wimbo wa 'Komasava' katika vipengele viwili, kwanza Video Bora (Komasava) na Mtumbuizaji Bora kutoka Afrika.

Hii sio mara ya kwanza kwa msanii Diamond kuingiza nyimbo zake katika tuzo hizo, utakumbuka kuwa mwaka 2020 aliingiza wimbo wake wa ‘Jeje’ na Baba Lao katika Kinyang’anyiro hicho na kuishia hatua ya kwanza iitwayo ‘Consideration’.


Remix ya wimbo wa ‘Komasava’ mpaka kufikia sasa ina zaidi ya watazamaji milioni 27 katika mtandao wa YouTube huku original yake ikiwa na watazamaji milioni 6.5.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags