Dawa 4 za kikohozi kutoka India zahusishwa na vifo vya watoto 66

Dawa 4 za kikohozi kutoka India zahusishwa na vifo vya watoto 66

Shirika la Afya Duniani (WHO) limechapisha tahadhari ya kimataifa kuhusiana na dawa nne za kikohozi zilizotengenezewa nchini India baada ya kuhusishwa na vifo vya watoto 66 nchini Gambia.

Aidha dawa hizo ni  Promethazine Oral Solution, Kofexmalin Baby Cough Syrup, Makoff Baby Cough Syrup na Magrip N Cold Syrup "zimehusishwa na majeraha mabaya ya figo na vifo 66 vya watoto." -WHO.

Hata hivyo WHO imeonya kuwa matumizi yao yanaweza kusababisha majeraha makubwa au kifo, haswa miongoni mwa watoto.

Sambamba na hayo, kampuni iliyotengeneza hizo dawa imeshindwa kutoa hakikisho kuhusu usalama wake, taarifa ya WHO ilisema.

Bidhaa hizo nne zilitambuliwa nchini Gambia, lakini "huenda zilisambazwa, kupitia masoko yasiyo rasmi, kwa nchi au kanda nyingine", iliongeza WHO, katika tahadhari iliyochapishwa kwenye tovuti yake.

Chanzo BBC.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Saphinia Suleiman

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, career, skills development and technology.


Latest Post

Latest Tags