Chris Brown akabiliwa na tuhuma za ubakaji

Chris Brown akabiliwa na tuhuma za ubakaji

Msanii Chriss Brown anadaiwa Kiasi cha Sh. Bilioni 46 na mwanadada Diddy aliyedai kuwa alibakwa na msanii huyo kwenye boti iliyokaribuni na nyumbani kwake huko Florida.

Diddy ambaye pia ni mwimbaji wa muziki amedai kuwa alibakwa na Chris Brown Desemba 30, 2020 ambapo Chris alitumia siku ya rafiki yake kumsihi afike nyumbani siku ya Miami’Star Island na alikubali kufanya hivyo.

Anadai Chris alimuuliza kama anahitaji kinywaji na kuambiwa aelekee jikoni.

Hata hivyo nyaraka za mahakama zinaeleza kuwa mwanamke huyo aliingia jikoni na Chris na kupewa kinywaji kilichochanganywa na dawa huku wakiendelea na mazungumzo na baada ya muda kidogo alianza kuhisi mabadiliko ya ghafla yaliyosababiha akapoteza fahamu.

Nyaraka hizo zinaendelea kueleza mwanamke huyo alijihisi amechanganyikiwa, kutokuwa sawa kimwili na kuanza kusinzia ndipo anadai Chris alimpeleka chumbani na kumbaka.

Kutokana na tuhuma hizo mwanamke huyo anadai Sh. Bilioni 46.2 akieleza kwamba kitendo alichofanyiwa kinamfanya kuwa na msongo wa mawazo.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags