Canada yakanusha kutoa fursa ya ajira kwa Wakenya

Canada yakanusha kutoa fursa ya ajira kwa Wakenya

Serikali ya Canada imekanusha ripoti kuwa Wakenya sasa wanaweza kusafiri hadi nchini humo kutafuta nafasi za kazi.

Haya yanajiri kufuatia tangazo la Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya Alfred Mutua Jumanne kwamba Wakenya sasa wataweza kwenda kuishi au kufanya kazi nchini Canada.

Mutua, ambaye alikuwa katika ziara rasmi nchini alisema alifanya mkutano na Waziri wa Uhamiaji, Wakimbizi na Uraia wa Canada (IRCC) Sean Fraser na kukubaliana kuhusu fursa mbalimbali za uhamiaji.

Pia alisema mchakato kwa wanaotaka kwenda Canada ni rahisi lakini unahitaji bidii. Taarifa potofu zinasambaa ambazo zinapendekeza kuwa programu maalum zinakaribisha wahamiaji wa Kenya.

Huu ni uongo, na programu za uhamiaji zilizotajwa hazipo," IRCC ilisema katika taarifa. IRCC ilisema kwa taarifa sahihi kuhusu jinsi ya kuhamia Canada, Wakenya wanapaswa kutembelea tovuti ya uhamiaji nchini humo.

Chanzo BBC






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags