Burna Boy ashinda tuzo ya msanii bora Africa

Burna Boy ashinda tuzo ya msanii bora Africa

Msanii maarufu barani Afrika Burna Boy, ameshinda tuzo ya msanii bora kutoka Afrika. Hii ni katika tuzo zilizofanyika huko Uingereza zinazojulikana kama MTV EMA.

Burna Boy amewabwaga wasanii wengine kutoka Afrika waliokua wakiwania tuzo hiyo kama vile Zuchu, Arya Starr, Tems, Black Sheriff na Musa Keys.

Tofauti na kipengele hicho, mwanadada Taylor Swift amevunja rekodi kwa kutwaa tuzo nne katika usiku huo wa MTV EMA.

Miongoni mwa tuzo aliyopata ni ya video bora kupitia wimbo wake wa “all too well.”


Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post