Mwanamuziki wa Bongo Fleva nchini Zuchu ameripotiwa kufikisha Subscriber milioni 4 katika mtandao wake wa Youtube.
Hatua hiyo imepelekea kuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kufikisha Subscriber milioni 4 huku nafasi ya pili ikishikwa na Nandy 1.6 milioni, Rose Muhando 1.2 milioni na nafasi ya nne ikienda kwa Diana Bahati mwenye 1.2 milioni.
Mbali na mtandao huo, ikumbukwe mapema mwaka jana kupitia jukwaa la kusikiliza na kuuza muziki alifikisha wasikilizaji milioni 300 akiwa msanii pekee wa kike Afrika Mashariki mwenye zaidi ya wasikilizaji milioni 200.
Lakini pia alifanikiwa kuweka rekodi nyingine kwa kuwa msanii wa kwanza wa kike Afrika Mashariki kufikisha idadi ya watazamaji (Views Mil 100) kupitia mtandao wa Youtube kupitia wimbo wa Sukari aliyouachia mwaka 2021.

Leave a Reply