Mkali wa Afrobeat kutoka Nigeria, Burna Boy, anaendelea kung’ara kimataifa kufuatia uwezo wake wa kuchanganya Afrobeat na miondoko mingine kama reggae, dancehall, na pop. Jambo linalomfanya awe kivutio kwa mashabiki ulimwenguni. Hizi ni baadhi ya rekodi alizobeba.
Mwaka 2020 alianza kuweka rekodi kwa kujaza uwanja wa O2 Arena, London, ukumbi ambao umekuwa ukitumiwa na mastaa wakubwa Marekani. Ambapo hatua hiyo ilithibitisha ukubwa wake na kuwa mmoja wa wasanii kutoka Afrika kuingia anga za kimataifa na kuweka rekodi hiyo.
Baada ya kujikusanyia kijiji chake mwaka 2020, alirudi tena 2021 kwa kishindo ambapo alifanikiwa kushinda tuzo ya Grammy katika kipengele cha Albamu Bora ya Muziki ‘Twice As Tall’. Ambapo ushindi huo uliongeza umaarufu wake na alikubalika kama mmoja wa wasanii wa Kiafrika wenye nguvu duniani.
Mwaka 2019-2020 alikoleza moto kwa kurudi na Tour ya "African Giant" ziara ambayo alijitambulisha na kuweka rekodi sehemu mbalimbali kama New York, Los Angeles, na Paris. Hakuishia hapo mwaka 2022 alijipata zaidi kwa kuujaza uwanja wa Spaceship unaoingia mamilioni ya mashabiki.
Kwa sasa msanii huyo anatembea na historia mpya ambayo ameiweka Aprili 18,2025 kwa kuwa msanii wa kwanza kutoka Afrika kujaza uwanja wa Stade de France unaochukua watazamaji 80,000 mjini Paris.

Leave a Reply