Waziri Mkuu Azindua Mfumo Wa Usimamizi Na Uendeshaji Kazi Za Sanaa

Waziri Mkuu Azindua Mfumo Wa Usimamizi Na Uendeshaji Kazi Za Sanaa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua mfumo wa Usimamizi na Uendeshaji Kazi za Sanaa unaojulikana TAUSI wa OR-TAMISEMI na AMIS wa BASATA ambao unaunganisha Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) na Taasisi nyingine hususani Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Akizungumza katika hafla ya kufungua Kikao Kazi cha 15 cha Maafisa Utamaduni na Maendeleo ya Michezo kilichofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, amesema mfumo huo utarahisisha urasimishaji, kuongeza mapato pamoja na uendeshaji shughuli za sanaa na kuweka kazi data ya wasanii na wadau wa sanaa.

"Hili ni jambo zuri sana na Watanzania tunatakiwa kuthamini na kulinda utamaduni wao kama msingi wa utambulisho wa taifa na urithi wa kizazi cha sasa na kijacho, kwani utamaduni ni silaha muhimu ya kujenga mshikamano wa kitaifa na kukuza uchumi kupitia sanaa na michezo," amesema.

Aidha, Majaliwa ameendelea kusema kuwa, mageuzi ya kisayansi na kiteknolojia duniani yameleta muingiliano mkubwa wa tamaduni, hivyo kuna haja ya kuwa makini ili mabadiliko hayo yapelekee mmomonyoko wa maadili miongoni mwa Watanzania hasa vijana huku akiwataka maafisa wa sekta hizo kuhakikisha kuwa msingi wa utamaduni wa taifa unaenziwa, unalindwa, na unarithishwa ipasavyo.

“Kamwe tusikubali kukumbatia tamaduni zinazokwenda kinyume cha maadili na ustaarabu wetu. Tusikubali kuwa watumwa wa tamaduni za kigeni ambazo zinadhalilisha utu wetu. Pamoja na umuhimu wa kujifunza mambo mazuri ya tamaduni nyingine ni lazima kuchuja nini cha kuchukua na nini cha kuacha,” amesema Waziri Mkuu Majaliwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags