Na Michael Anderson
Adui mkubwa wa maisha ya mtu ni woga. Na woga husababishwa na hofu, ambayo ni kiashilia cha kukutaka uwemakini.
Hofu inapatikana kwenye kitengo cha usawa (kiasi). Mtu anapokuwa mtumwa wa hofu anaitwa mwoga. Moja ya maadui wakubwa wa mtu ni woga. Ukiachilia mbali adui mwingine ambaye huwasumbua watu, adui binafsi, woga ni mbaya sana.
Mara nyingi kitu ambacho unakiogopa huwa hakina ukweli ndani yake, yaani si sawa na vile ambavyo unaogopa. Kumbuka hofu huja ili kukupa tahadhari tu.
CHUKUA HII
Chochote ambacho unakiogopa ukikumbana nacho huwezi kukiogopa tena. Haijalishi ni hatari kiasi gani?
Kwa hiyo kitu cha kuogopa katika maisha ni hofu yenyewe. Ogopa hofu isije ikakupeleka kwenye woga, lakini usiogope hofu kwani si kitu ambacho ni kweli.
Angalia ni maeneo gani ambayo yanasumbua na kukutia hofu wakati wote, halafu jiulize. Je! ni kweli napaswa kuogopa? hiyo angalia ni kitu gani kinakufanya uwe mtumwa wa hicho.
Changamoto ni kitu ambacho kinajitokeza kwenye maisha wakati wote. Changamoto ni kama kifundo cha muwa na utamu wake.
Kifundo cha muwa ni kidogo ukilinganisha na sehemu ambayo ni tamu. Hivi ndivyo changamoto na raha kwenye maisha zilivyo kama muwa.
Angalia ushindi usiangalie matatizo, popote utakapopita kwa sababu ushindi ni mkubwa kuliko changamoto. Kipindi cha changamoto hakiitaji Hofu yoyote songa mbele ivuke hofu ya mafanikio.
Leave a Reply