PEkkachai Tiranarat na Laksana, wanandoa wa muda mrefu kutoka Thailand waliowahi kuvunja rekodi ya Guinness World Record kwa kubusu muda mrefu zaidi mwaka 2013 ambapo walibusiana kwa masaa 58 na dakika 35 wameachana baada ya kudimu kwa muongo mmoja.
Wakati alipokuwa kwenye podikasti ya ‘BBC Sounds Witness History’, Ekkachai hakutoa sababu wala maelezo ya kina kuhusu kuachana kwao huku akijikita zaidi kuelezea mazuri waliyoyafanya pamoja.
Hata hivyo, walieleza kuwa, licha ya kutengana wanajivunia mafanikio yao kama wapenzi, ikiwa ni pamoja na kuweka rekodi ya Guinness World Record kwa kubusu kwa muda mrefu zaidi.
alielezea pia rekodi hiyo ilikuwa ni tukio la kipekee maishani mwao, lakini baada ya karibu muongo mmoja pamoja, walijua ni wakati wa kila mmoja kutafuta njia tofauti katika maisha yao.

Leave a Reply