Kawaida tasnia ya muziki inaambatana na masuala ya fasheni na mitindo. Na hii ni kutokana na mchango wa mwonekano katika katika kukuza brand ya msanii.
Hii imejionesha katika Tuzo za Muziki za Trace zilizofanyika usiku wa Februari 26, 2025 Zanzibar kisiwani Unguja, ambapo wasanii mbalimbali walilipamba zuria la buluu kwa mitoko ya aina yake.
Mitupio ya wasanii kwenye usiku wa Trace
Diamond Platnumz
Katika tuzo hizo mwanamuziki Diamond alitokea akiwa na Suruali ya Cargo nyeusi ambayo ilikuwa na koti lake jeusi. Akivalia juu ya flana nyeupe.
Nyota huyo wa muziki Bongo kichwani alikuwa ametupia durag kwa ajili ya kufunika rasta zake. Diamond amekuwa miongoni mwa wasanii ambao wanapendeza sana katika matukio mbali mbali.
D Voice
Dvoice ambaye ni msanii kutokea lebo ya Wasafi katika tuzo hizo alitokea akiwa katika mwonekano wa kitofauti ambao umewashangaza wengi kwenye mitandao ya kijamii.
Hiyo ni baada ya kuingia na nguo nyeusi juu mpaka chini. Ikiwa ni pamoja na suruali, shati na kiatu. Huku mabegani nguo yake ikinakshiwa na kitu kama puto ambalo limechora muonekana wa kopa.
Zuchu
Msanii mwingine ambaye alionekana katika mwonekano uliozua gumzo ni Zuchu ambaye alitinga na gauni refu lenye rangi ya chungwa.
Kutokana na mwonekano wake wengi wamekuwa wakilijadili kwa kudai lipo katika mwonekano wa kuvaliwa na bibi harusi.
Nandy
Hata hivyo mwanamuziki Nandy hakubaki nyuma kwenye suala la mwonekano usiku huo. Ambao pia aliingia na gauni refu la kijani ambalo lina mtindo wa nguva.
kwa mujibu wa maelezo yake alisema imemchukua wiki mbili kuliandaa vazi hilo kwa ajili ya Trace Music Awards.
Seangarreette
Huyu ni mwandishi wa nyimbo za Rihanna, Usher Raymond na wasanii wengine. Yeye alitokea amevalia fulu jeans ya bluu mpauko . Yaani juu mpaka chini ikiwa na nakshi za kung'a. Hivyo basi vazi hilo lilimpa mwonekano bomba
Jux
Juma Jux kama kawaida yake, hajawahi kutokea kinyonge popote. Katika hafla hiyo ameendeleza ubabe wake akiwa na mkewe.
Jux alivalia suti nyeusi yenye ufito mweupe kwenye mifuko na sehemu za vishikizo. Pia ilikuwa na nakshi nakshi za kung'aa. Kisha akatupia na miwani yenye rangi nyeusi.
Upande wa bibie Priscilla alivalia gauni ndefu ambayo inamikono mifupi, ikiwa na mtandio ambao umefunika kichwa. Wote walitoka bomba
Leave a Reply