Bila nidhamu binafsi ngumu kutoboa kimaisha

Bila nidhamu binafsi ngumu kutoboa kimaisha

Na MICHAEL ANDERSON

Nidhamu maana yake ni utaratibu au sheria anayojiwekea mtu au kuwekewa mtu katika kufanya au kutofanya kitu ama jambo fulani.

Mara nyingi nidhamu humwongoza mtu na kumwekea mipaka kwa baadhi ya vitu kuvifanya au kutokuvifanya ama kwa kupenda au kutopenda.

Nidhamu ziko za aina mbili, nidhamu binafsi anayojiwekea mtu  kwa makusudi ya kutimiza malengo fulani aliyojiwekea katika maisha yake.

Na kuna nidhamu inayowekwa na kikundi, taasisi, kampuni au serikali ya nchi kwa madhumuni maalumu na hata jamii fulani

Leo tunaangalia zaidi katika nidhamu binafsi. Nidhamu binafsi ndio imekufanya wewe uwepo hapo ulipo na uwe hivyo ulivyo. Ni kutokana na nidhamu binafsi ndiyo  imekufanya ufanikiwe au usifanikiwe katika maisha yako.

Nidhamu binafsi ndiyo inayomwongoza mtu katika kufanya maamuzi sahihi au yasiyo sahihi katika maisha yake.

 

Zifuatazo ni faida za mtu kuwa na nidhamu binafsi

  1. Nidhamu binafasi humfanya mtu kujitambua yuko wapi, ni nini wajibu wake katika maisha yake na jamii inayomzunguka. Hii inaleta matokeo chanya katika sehemu uliyopo
  2. Humwongoza mtu katika kufanya maamuzi sahihi katika maisha yake kwani humfanya atafakari kwanza hasara na faida ya kile anachotaka. Kabla ya kulifanya na maamuzi hayo huwa na faida sana katika maisha yako binafsi na si wengine
  3. Humfanya atimize malengo yake kirahisi kwa sababu hufikiri kabla ya kufanya mambo.
  4. Nidhamu binafsi humfanya mtu kupendwa na watu kwa sababu ya kufanya vitu sahihi na vyenye uhakika.
  5. Humfanya mtu asikurupuke na kuiga vitu asivyo na uhakika navyo. Kwa sababu ya mipaka mtu uliyojiwekea
  6. Humfanya mtu kutimiza majukumu yake kwa wakati.

Hutakua na viporo katika malengo yako utatimiza kwa wakati kwa sababu unajua nini unatakiwa kutimiza kwa wakati huo na faida ya kutimiza hilo .

  1. Humfanya mtu kujiamini na kuondokana na hofu katika maisha

Nidhamu binafsi ukiizingatia utaishi maisha ya furaha sana kwa umri huu. Wa ujana na hasa maisha ya vyuoni.

  1. Humfanya mtu kuwa na matumizi mazuri ya muda na pesa.

Kwenye pesa ndiyo muhimu sana kwa maana pesa haiitaji utovu wa nidhamu itakunyoosha hasa pesa za boom wanafunzi wengi wanapata changamoto hawana nidhamu binafsi na pesa za boom. Matumizi yasiyo ya lazima epuka acha starehe chuoni umefuata elimu

  1. Humfanya mtu kujituma na kufanya kazi kwa bidii.

Kwa sababu utakua na set up goals lazima uongeze juhudi na bidii katika kila nyanja ili kufikia malengo yako. Nidhamu pekeee itakupa moyo wa kujituma kufikia mbali zaidi hivyo zingatia sana maadili binafsi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags