Kwa mujibu wa utafiti uliochapishwa kutoka tovuti ya ‘European Heart Journal’ unaonesha kuwa kufurahia kikombe cha kahawa asubuhi kunaweza kupunguza hatari ya magonjwa ya moyo na vifo vya ghafra kwa ujumla.
Utafiti huo, uliofanywa na Dkt. Lu Qi na timu yake katika Chuo Kikuu cha Tulane, ulitathmini data kutoka kwa watu wazima zaidi ya 40,000 walioshiriki katika Uchunguzi wa Kitaifa wa Afya na Lishe nchini Marekani kati ya mwaka wa 1999 na 2018.
Matokeo yanaonyesha kuwa wanywaji wa kahawa asubuhi walikuwa na uwezekano mdogo kwa 31% wa kufariki kutokana na ugonjwa wa moyo ikilinganishwa na wale waliokunywa kahawa siku nzima au ambao hawakunywa kahawa kabisa.
Leave a Reply