Sugu: Msanii wa kwanza Bongo kumiliki Honda Accord Inspire

Sugu: Msanii wa kwanza Bongo kumiliki Honda Accord Inspire

Peter Akaro

Msanii wa Hip Hip Bongo na Mwanasiasa kwa sasa, Joseph Mbilinyi 'Mr. II 'Sugu' alitoka rasmi kimuziki mwaka 1993, hivyo ana miaka 32 katika tasnia ambayo anajivunia kwa kufanikisha kile anachoita kurasimisha muziki.

Sugu ambaye anatamba na ngoma kama 'Taita' toka Tongwe Records, ndiye msanii wa kwanza Bongo kuanza kulipwa vizuri ambapo kwa miaka hiyo alikuwa akichukua Sh100,000 kwa shoo.

Rafiki yake toka Marekani ambaye alikuwa akimkubali kimuziki ndiye aliyempa jina la 2Proud kufuatia kali zake za kila mara; 'Am too proud of you', katika kufupisha ndio akaja na jina hilo, 2Proud, kisha likafuata, Mr. II.



Jina la Sugu lilikuja kuanzia kwenye albamu yake ya nne, Nje ya Bongo (1999) na ya tano, Millennium (2000) baada ya watu kuona anazidi kukomaa na muziki na mfululizo wa albamu, ndio wakaamua kumuita Sugu.

Sugu aliamua kuja Dar es Salaam kwa ajili ya kusomea kozi ya 'Clearing and Forwading' katika Chuo cha Equatorial Training College kama alivyomueleza Baba yake ila lengo lake lilikuwa na kutafuta nafasi ya kufanya muziki.

Mara ya kwanza Sugu kutumbuiza na kubaina ana uwezo mkubwa ni mwaka 1992 ambapo ilikuwa ni kwenye Mahafali ya Chuo cha Walemavu pande Yombo, Dar es Salaam.

Sugu ndiye msanii wa kwanza kumlipa vizuri Prodyuza, Master J ambaye wakati huo alikuwa anarekodi kwa Sh50,000 lakini Sugu akamlipa Sh100,000 ambapo walianza kufanya kazi kwenye albamu yake pili, Ndani ya Bongo (1996) na kuendelea.

Mwaka 2000 Sugu alishinda Tuzo za Muziki Tanzania (TMA) kama Msanii Bora wa Hip Hop na tuzo hiyo alikabidhiwa na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete ambaye kwa wakati huo alikuwa Waziri wa Mambo ya Nje.

Sugu ndiye msanii kwanza Bongo kumiliki chombo cha habari (print media), ambapo mwaka 2004 alikuwa na gazeti lake linalokwenda kwa jina la Deiwaka.

Miongoni mwa albamu alizotoa Sugu ni Ni Mimi (1995), Ndani ya Bongo (1996), Niite Mr II (1998), Nje ya Bongo (1999), Millennium (2000), Muziki na Maisha (2001), Itikadi (2002), Sugu (2004), Coming of Age-Ujio Wa Umri (2006) na VETO (2009).

Sugu aliamua kuuza mwenyewe albamu yake ya nne, Nje ya Bongo (1999) baada ya kuona ubabaishaji katika soko na ndio ilimuingia fedha nyingi zaidi hadi kununua gari yake aina ya Honda Accord Inspire na kuwa msanii wa kwanza Bongo kuimiliki.

Katika kumkubali Rapa wa Marekani, Jay Z kimuziki na kibiashara, Sugu amempa mtoto wake wa pili jina la Shawn ambalo ndio la kuzaliwa la Jay Z, ikumbukwe Sugu ni msanii wa pili Bongo kufanya hivyo, wa kwanza ni Marehemu Godzilla.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags