Sababu Wanasoka Kupendelea Kuoa Wanamitindo

Sababu Wanasoka Kupendelea Kuoa Wanamitindo

Kwenye ulimwengu wa mapenzi, inaonekana nyota wengi wa mpira wa miguu wanavutiwa zaidi na wanamitindo. Na hii siyo tu kwa Aziz Ki ambaye Februari 16, 2025 alifunga ndoa na mwanamitindo Hamisa Mobetto.



Nje ya Bongo wapo mastaa wa soka waliozama na waliowahi kuzama kwenye ulimwengu wa huba na wanamitindo kama ilivyotokea kwa David Beckham na mkewe Victoria Beckham, Peter Crouch na Abbey Clancy.

Cristiano Ronaldo na Georgina Rodríguez, Lionel Messi na Antonela Roccuzzo huku Sergio Ramos akimuoa mwanamitindo Pilar Rubio, Neymar na Marquezine.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Breaking Thelines, Soccer Sports Narkive na Goalball Live inaelezwa kuwa kati ya sababu ya wachezaji kuamua kuchagua upande huo wa mapenzi ni kupewa umakini na jamii. Kwani wachezaji wengi wanaamini kuwa kuoa mwanamitindo au mwanamke mrembo kunaongeza hadhi katika jamii na kuimarisha kutambulika kwake katika vyombo vya habari.



Kuendana katika mtindo wa maisha

Mara nyingi wachezaji wa mpira wa miguu na wanamitindo wanaendana mitindo ya maisha kwani wanamitindo hutumia muda wao mwingi kupata madili mengi ya matangazo kutoka kwenye makampuni. Ambapo nyota wengi wa mpira wa miguu wanachukulia hatua hiyo kama fursa kwao ya kujipenyeza katika maadili ya watu wanaowaoa ili kuendelea kutambulika zaidi.

Kubebana katika maisha

Wachezaji wengi wa mpira wa miguu wana kazi inayoisha katika kipindi kifupi kwa sababu ya mabadiliko ya mwili, majeraha, au umri kwani wachezaji wengi huacha kufanya kazi zao wakiwa na umri kuanzia miaka 35 hadi 40.



Lakini kwa wanamitindo kazi zao zinaendelea kuwatambulisha katika jamii hata wakiwa wazemeka. Hivyo basi sababu nyingine wachezaji mpira kuoa wanamitindo wanaamini kuwa watakapostaafu kucheza mpira basi wana nafasi ya kuendelea kujulikana zaidi kwa jamii wakitumia migongo ya wake zao ambao ni wanamitindo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags