Ex Wa Elon Musk Alia Kutopata Huduma Za Watoto

Ex Wa Elon Musk Alia Kutopata Huduma Za Watoto

Grimes ambaye ni mwanamuziki na mzazi mwenza wa tajiri na mmiliki wa mtandao wa X, Elon Musk, anadai kuwa tajiri huyo hajiuhusishi na mahitaji ya mtoto huku akidai kuwa hapokei simu na wakati mtoto anaumwa.

Msanii huyo alichapisha ujumbe kupitia mtandao wa X akimtaka Elon kushughulikia matibabu ya mtoto kwa haraka.

“Pole kwa kufanya hili hadharani lakini hali hii haiwezi tena kupuuziliwa mbali. Inahitaji umakini wa haraka. Ikiwa hutaki kuzungumza na mimi, tafadhali unaweza kumteua au kumajiri mtu anayekubalika ili tuweze kusonga mbele kutatua hili? Hili ni la dharura, Elon.

Hajibu simu wala barua pepe na hajatokea kila nilipo omba tukutane, na mtoto wetu atapata uharibifu wa maisha marefu ikiwa hatajibu haraka kwa hivyo ninahitaji msaada wenu,” amesema Grimes.

Grimes na Musk wana watoto watatu pamoja, akiwemo X Æ A-Xii ambaye hivi karibuni alionekana Ikulu ya White House, Exa Dark Sideræl, na Techno Mechanicus. Haijulikani ni mtoto gani anayeongelewa katika posti ya Grimes.

Wawili hao walikuwa katika uhusiano kuanzia mwaka 2018 na kutemana 2022 huku sababu ya kuachana kwao ikitajwa kuwa mmoja wao alikuwa na matatizo ya kiafya.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags