Mwonekano Wa Ariana Wamuweka Tate Matatani

Mwonekano Wa Ariana Wamuweka Tate Matatani

Bibwa wa zamani wa kickboxing Andrew Tate, amejikuta akikalia kuti kavu kwenye mtandao wa X (Zamani Twitter). Baada ya kuchapisha ujumbe unaokosoa mwonekano wa mwanamuziki na mwigizaji Ariana Grande.

Bingwa huyu wa zamani ambaye mwaka 2022, alidakwa na polisi kwa tuhuma za biashara ya binadamu, ubakaji na kuunda genge la kihalifu la kuwanyanyasa wanawake kimapenzi. Katika ujumbe wake alidai hatoendelea kumpenda Ariana kutokana na mwonekano alionao sasa.

"Pole Ariana Grande, umekuwa hauvutii sitaendelea kukupenda tena, umekuwa kama mtumiaji wa madawa ya kulevya,"

Hata hivyo aliendelea kutoa maoni yake chini ya picha ya Ariana ambayo hivi karibuni ilisababisha hofu kwa mashabiki kuhusu afya yake.

Kutokana na maoni hayo mashabiki walionekana kumkingia kifua Ariana kwa kumvaa Tate kwa maoni yake waliyoyaita ya kiovu huku baadhi yao wakiandika.

"Kwa nini wanaume wanafikiri kuwa ni sawa kutoa maoni kuhusu miili ya wanawake?"

"Huu ni ujumbe usiofaa niliouona leo. Vipi watu kama hawa bado wanapata nafasi ya kuwepo katika programu hii ya X?"

"Yeye ni maarufu zaidi kuliko wewe, ana pesa zaidi, mafanikio zaidi, ana sifa nzuri, na hajawahi kuwa jela,"

Utakumbuka kuwa mwili wa msanii huyo ulizua mijadala baada ya kuonekana kudhoofika na uliopungua tofauti na alivyokuwa awali.Kwa mara ya kwanza wengi waliona mwonekano wake mpya katika uzinduzi wa filamu ya Wicked iliyozinduliwa mwishoni mwa 2024.

Ariana Grande amewahi kushinda tuzo kama MTV Europe Music Awards,MTV Italian Music Awards, MTV Millennial Awards,MTV Millennial Awards Brazil na nyingine nyingi. Hadi sasa ana zaidi ya tuzo 30 kwenye kabati lake. Na kwa sasa anawania tuzo ya Oscars 2025 zitazotolewa Machi, 3. Akiwa katika kipendele cha Best Actress in a Supporting Role kupitia filamu ya Wicked.

Pia tuzo nyingine anayowania kwa mwaka huu ni Golden Globe Awards 2025, kipengele cha Best Supporting Actress – Motion Picture kupitia filamu hiyohiyo ya Wicked. Tuzo nyingine ni BAFTA Awards kupitia filamu hiyo hiyo.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags