Mwanamuziki wa marekani T-pain anaripotiwa kuuza katalogi yake ya uchapishaji (mkusanyiko wa nyimbo) pamoja na baadhi ya masters zake za muziki kwenye kampuni ya HarbourView Equity inayohusiana na uwekezaji katika ubunifu, na masuala ya vyombo vya habari.
T-pain ameelezea furaha yake katika ushirikiano huo wa kuhifadhi muziki wake, akijivunia juhudi zake katika kufanya kazi kwa muda wote huku akisema hana mpango wa kusitisha mkataba huo hivi karibuni.
"Nimefurahishwa na sura hii inayofuata ya kushirikiana na HarbourView Equity wanaposaidia kuhifadhi urithi wa muziki wangu. Orodha hii inawakilisha miaka ya bidii, ubunifu, na wakati usioweza kusahaulika, na ninashukuru kuona ikiendelea kufikia urefu mpya. Sina mpango wa kuacha hivi karibuni,” alisema mwanamuziki huyo.
Mwanzilishi wa kampuni ya uwekezaji ya HarbourView ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji, Sherrese Clarke alitoa maoni na amemkaribisha kwa furaha msanii huyo katika kushirikiana kufanya nae kazi.
“Tunafuraha kumkaribisha T-Pain, mfuatiliaji wa kweli katika tasnia ya muziki, kwa familia ya HarbourView. Ustadi wake wa maono na ubunifu umeacha alama isiyoweza kufutika kwenye muziki wa kisasa, na hatuwezi kungoja kushirikiana na kukuza urithi wake wa ajabu zaidi,” amesema Clarke.
Tangazo hilo pia linaambatana na maadhimisho ya miaka 20 ya nyimbo kadhaa za T-Pain kama vile Buy U a Drank (Shawty Snappin'), Bartender akishirikiana na Akon,I'm N Luv (Wit a Stripper) akiwa na Mike Jones, Flo Rida's Low, na I'm Sprung.
T-Pain anaunga tela la orodha ya wasanii wa Hip-Hop ambao wameuza katalogi yao kwa HarbourView Equity. Akiwemo Wiz Khalifa ambaye alishirikiana na kampuni hiyo kibiashara ikihusisha mauzo ya muziki wake kwa mwaka 2023. Ambapo nyimbo kama vile "See You Again," "Black & yellow," na "The Thrill aliwauzia HarbourView Equity.
Lakini pia, msanii Nelly mwaka 2023 aliuza nusu ya katalogi yake kwa 'HarbourView Equity Partners' kwa kiasi cha dola 50 milioni kama ilivyoripotiwa, biashara hiyo ilijumuisha mauzo ya nyimbo kama Ride Wit Me, Dilemma, na Hot in Herre,

Leave a Reply