Baada ya msanii wa Bongo Fleva, Lady Jaydee kufanya Cover ya wimbo wa 'Goodness of God' wa Cecewinans mashabiki wamtaka kufanya nyimbo za Injili kwa wingi.
Jaydee amesema amefanya cover ikiwa kama shukrani ya kutimiza miaka 25 kwenye kiwanda cha muziki.
"Nimefanya hii Cover ya Cecewinans Goodness Of God ikiwa ni shukrani zangu kuvuka kila hatua Na kufikisha miaka 25 kwenye kiwanda cha muziki na burudani. Sifa na utukufu ni kwa alie juu," amesema Jaydee.
Mashabiki wengi wameonekana kupendezwa na uwezo mkubwa aliouonesha msanii huyo kwenye wimbo huo huku wengi wakihitaji afanye hata album ya nyimbo za injili.
Maureen Mwaisa, ambae ni shabiki kupitia upande wa koment ameandika "Jide nyimbo nyingine zinazoingiq sauti yako kusikika how powerful it is ... please tuletee nyimbo yako kwa sauti ya kiwango hiki" amesema.
Lakini pia, MC Pilipili "Jidejaydee una kitu kikubwa sana Gospel bado inakudai kitu fulani hata albamu tu itainua mioyo ya watu" amesema Pilipili.

Leave a Reply