Mfahamu Mtoto Asiyehisi Njaa, Maumivu Wala Uchovu

Mfahamu Mtoto Asiyehisi Njaa, Maumivu Wala Uchovu

Kupata maumivu, uchovu pamoja na njaa ni hali ya lazima kwa kila mwanadamu, lakini hili ni tofauti kwa binti aitwaye Olivia Farnsworth kutoka Uingereza ambaye anatambulika kwa jina la utani kama ‘Bionic Girl’ kutokana na hali yake inayomfanya asihisi maumivu, njaa wala uchovu.

Wataalamu wa afya wanasema mtoto huyo anasumbuliwa na ugonjwa ambao ni nadra kwa binadamu unaotokana na kupoteza sehemu ya vinasaba (chromosome 6 deletion) katika mwili wake.

Moja ya tukio la ajabu ambalo liliwashangaza wengi wakati alipokuwa na umri wa miaka 7 alipata ajali ya kugongwa na gari na kuburuzwa kwa takribani mita kumi lakini cha ajabu hakulia wala kuhisi maumivu na badala yake alisimama na kumfuata mama yake.

Hata hivyo baada ya kupelekwa hospitali, madaktari walimtibu baadhi ya majeraha huku wakimtunga jina la utani ‘Bionic Girl’ kutokana na uimara wake.

Aidha mama yake anasema changamoto kubwa ni kumlinda dhidi ya matukio yatakayomsababishia majeraha pamoja na kumkumbusha kula kwa sababu anaweza kukaa muda mrefu bila kula chakula na haoneshi dalili yoyote. Lakini pia kumsaidia kupata usingizi kwani hupata usingiza saa chache usiku na anaweza kukaa macho hadi siku tatu mfululizo bila kuchoka.

Kwa sasa, familia yake inaendelea kumsaidia na kuhakikisha anapata maisha ya kawaida kadiri inavyowezekana licha ya hali hiyo ya kipekee.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags