Msanii wa Bongo Fleva Treyzah ameendelea kuupiga mwingi katika muziki huku akiachia ngoma yake mpya iitwayo ‘Sitaki Tena Mapenzi’.
Ufundi wake wa kuchora nyimbo za mapenzi umeendelea kuaminisha kipaji chake kwa mastaa waliomtangulia akiwemo Belle 9 na King Kaka ambaye amempa maua yake baada ya kusikiliza .
Akizungumza na mwananchi Treyzah ameweka wazi changamoto anazopitia ikiwemo kukosa ushirikiano kutoka kwa wasanii wanaofanya vizuri.
"Nadhani kwenye mapokezi sapoti ya watu ambao wapo kwenye mifumo ni watu ambao wanahofia aina hii ya muziki ninayofanya. Kwa hiyo kuna kukatishwa tamaa unakuta wanasema kwanini usifanye sound nyingine.
“Lakini mimi naona ninachokifanya kina kitu na ndiyo maana napambania nisipofanya mimi watu wengine hawatofanya pia kwa sababu kinachohitajika ni kufanya kitu cha utofauti na bora ,"amesema Treyzah
Treyzah ameongezea kuwa licha ya kutopewa sapoti na baadhi ya mastaa, mapokezi anayopata kwa mashabiki yanampa nguvu.
Licha ya Treyzah kutambulika kupitia muziki wa R&B lakini amewahi kuachia wimbo wa Amapiano uitwao Karanga akimshirikisha Chino Kidd , amesema hata alivyotoa wimbo huo bado aliendelea kusikika kama msanii wa R&B.
" Uzuri wangu naweza nikaimba piano na saundi yangu ni ileile utaisikia tu naweza nikaimba kwenye piano na tone ikawa ya amapiano lakini sauti yangu ya R&B. Yaani popote nakuwa najisimamia sibadilishi uhalisia wangu nabaki palepale ," amesema Treyzah.
Hata hivyo, msanii huyo amesema bado anaimani na R&B kwenye majukwaa makubwa ya muziki huku akizungumzia alichofanya Bien kwenye Trace Music Awards zilizofanyika Zanzibar Februari 26, 2025.
"Perfomance ya muziki huu ni nzuri umeona kama alichofanya Bien kanyoosha sana ameonesha R&B ni muziki mkubwa sio kwenye live au sound," amesema Treyzah.
Amesema msanii wa Kenye King Kaka kuukubali muziki wake ni kiashiria cha kufanya vizuri.
“Ni wazi kuwa muziki wangu na Bongo Fleva inasogea sasa nje ya mipaka ya Tanzania collabo hiyo na King Kaka ni heshima na inanipa chachu na motisha ya kuendelea kufanya zaidi, kwahiyo watu waendelee kusapoti na mimi naahidi kutowaangusha,” amesema Treyzah.
Leave a Reply