Mashabiki wanataka album mpya kutoka kwa Rihanna

Mashabiki wanataka album mpya kutoka kwa Rihanna

Msanii kutokea nchini Marekani Rihanna, ambaye hajatoa albamu mpya tangu alipoachia album yake ya 'Anti' 2016, alionekana katika studio ya kurekodia huko Jijini New York Jumamosi, Januari 18, 2025

Sasa, baadhi ya mashabiki wa staa huyo ambae ni mshindi wa tuzo za Grammy kwa mara tisa wanabashiri kuwa huenda albamu mpya kutoka kwa staa huyo ikawa karibu kutoka.

Utakumbuka Rihanna katika mahojiano aliyoya fanya na 'Entertainment Tonight' Juni 2024, aliwahakikishia mashabiki kwamba albamu yake ya tisa ya studio itakuja lakini anataka kuifanya kwa mtazamo mpya kulingana na hali yake ya kimaishani kwa sasa.

"Nadhani muziki huo kwangu, ni uvumbuzi mpya, nimegundua mambo mapya Nimekuwa nikifanya kazi kwenye albamu mpya kwa muda mrefu kiasi kwamba niliweka mambo hayo yote kando na sasa niko tayari kurejea studio" alisema Rihanna.

Hata hivyo Rihanna aliongezea kuwa anataka kurejea na kusikiliza mambo upya kimtazamo na kuona kile kinachofaa na kile ambacho kitakuwa sawa kulingana na maisha yake.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags