Ben Paul afunguka kuhusu ukimya wake kwenye muziki

Ben Paul afunguka kuhusu ukimya wake kwenye muziki

Nyota wa muziki wa RnB nchini, Ben Pol amesema bado yupo sana katika fani hiyo licha ya ukimya wa muda mrefu uliotokana na kuamua kujipa likizo ya kutoachia kazi mpya yoyote.

Mara ya mwisho kwa Ben Pol kuachia ngoma mpya ilikuwa ni mwaka 2023 alipotoka na 'Iam in Love' na akizungumza na Mwanaspoti alisema, licha ya kuwa kimya hakuna mtu anaweza kumzuia kufanya muziki jinsi yeye anavyotaka au kuchukua nafasi yake kwa sababu muziki anaofanya yeye ni wa kipekee.

“Ninaweza kurudi muda wowote katika muziki, sisemi kuwa nitakaa muda mrefu bila kutoa wimbo kwa sababu kuna vitu nilitakiwa kuvifanya lakini sikuvifanya ambavyo ni mapumziko, kwa hiyo nimejipa muda wa kujitathmini kwani nimeandika nyimbo kibao, zinazosubiri tu muda wa kuziachia hadharani,” alisema.

Staa huyo wa Moyo Mashine, Maneno, Nikikupata na ngoma nyingine kali, aliongeza kwa kusema kwake kimya si kuishiwa mashairi bali ni hali ya kutunza heshima kwa mashabiki kwani idadi kubwa ya wasanii wanaofanikiwa kimuziki hutumia muda mwingi kufikiria vitu vipya ili kuboresha kazi tofauti na wale wanaokurupuka kutoa wimbo ndani ya muda mfupi.

“Unajua baadhi ya mashabiki wamekuwa na fikra potofu, wanapoona msanii yupo kimya akili zao zinawatuma kwamba kaishiwa wakati sivyo, na kukurupuka mara nyingi kumekuwa kukimaliza vipaji vya wasanii kwa haraka na kujikuta hawadumu kwenye fani zao," alisema Ben Pol.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags