Kumbe MJ aliokoka wiki mbili kabala ya kifo chake

Kumbe MJ aliokoka wiki mbili kabala ya kifo chake

Inaelezwa kuwa Mfalme wa muziki wa Pop Michael Jackson, alikuwa si tu mtu aliyegusa mioyo ya watu kupitia muziki wake bali alimpenda Mungu wakati wote.

Kabla ya kifo chake Juni 25, 2009, taarifa ziliripotiwa kuwa MJ aliwahi kuonesha nia ya kubadilisha maisha yake ya kiroho kwa mujibu wa watu wake wa karibu, ikiwa pamoja na familia yake na viongozi wa dini, Michael alimrudia Mungu wiki mbili kabla ya kifo chake.

Naye mchungaji Al Sharpton ambaye aliwahi kuwa karibu na MJ alieleza kuwa nyota huyo alikuwa akipitia kipindi kigumu cha maisha yake huku akitaja onesho la mwisho la msanii huyo lililojulikana kama ‘This Is It’ kumtesa kiimani na kiroho.

Aidha kwa upande wa familia yake hasa dada yake Rebbie Jackson alieleza kuwa Michael aliomba sana na kubatizwa upya kabla ya kifo chake huku mama yake Katherine Jackson akieleza namna alivyomshuhudia mwanaye akimrudia Mungu kwa unyenyekevu mkubwa.

Mbali na ndugu wa karibu pamoja na familia katika mahojiano aliyoyafanya na aliyekuwa mtayariashaji wa muziki wa MJ, Rodney "Darkchild" Jerkins alidai kuwa nyota huyo alimpenda Mungu hasa nyakati za mwisho za uhai wake.

“Ninaamini Michael alikuwa na uhusiano na Bwana. Najua kwa uhakika kuwa alimkubali Kristo moyoni mwake. Alimpenda Mungu sana kabla ya kifo chake,” alisema Darkchild

Michael Jackson alifariki dunia Juni 25,2009, akiwa na umri wa miaka 50, jijini Los Angeles, sababu ya kifo chake ikitajwa kuwa ni overdose ya dawa ya usingizi iitwayo propofol, ambayo alipewa na daktari wake binafsi, Dr. Conrad Murray.

Enzi za uhai wake Michael alitamba na ngoma mbalimbali ikiwemo Billie Jean, Thriller, Beat It, Smooth Criminal, Black or White, Man in the Mirror, Don’t Stop ‘Til You Get Enough ambao ulikuwa wimbo wake wa kwanza tangu aondoke kwenye kundi la familia.

Kutokana na mafaanikio yake mwongozaji Antoine Fuqua amepanga kuleta filamu ya maisha halisi ya msanii huyo iitwayo ‘Michael’ ambayo itachezwa na mpwa wake Jaafar Jackson ikitarajiwa kutoka Aprili 2026 au 2027.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags