Kanye West Azuiwa Kuingia Australia Kisa Wimbo

Kanye West Azuiwa Kuingia Australia Kisa Wimbo

Mwanamuziki kutoka Marekani Kanye West ambaye kwa sasa anajitambulisha kama ‘Ye Ye’, amezuiliwa rasmi kuingia nchini Australia baada ya serikali kufuta visa yake kufuatia na kauli za chuki alizozitoa dhidi ya Wayahudi.

Waziri wa Masuala ya Ndani wa Australia, Tony Burke, ametangaza kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na wimbo wa Ye uitwao ‘Heil Hitler’, aliouachia Mei mwaka huu, ambao umetajwa kuwa na maneno ya chuki.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa Waziri, Ye alikuwa na visa ya muda mfupi, lakini serikali iliamua kuifuta kwa misingi ya ulinzi wa maadili ya taifa, sambamba na msimamo wa nchi dhidi ya kauli zinazochochea chuki au kuunga mkono siasa za kibaguzi.

“Hatuhitaji kuingiza aina hiyo ya chuki nchini mwetu, Kuna mipaka ya kile tunachokikubali kama uhuru wa kujieleza,” alisema Waziri Burke.

Hatua hiyo pia imeungwa mkono na mashirika ya kijamii kama vile Australian Jewish Association, ambayo yalitoa malalamiko rasmi kuhusu maudhui ya wimbo huo, yakitaka Ye asiruhusiwe kuingia nchini humo.

Hii si mara ya kwanza kwa Kanye kukumbwa na ukosoaji kutokana na kauli zake tata awali amewahi kukosolewa na kufungiwa na majukwaa mbalimbali kwa kauli zinazodaiwa kuwa za chuki dhidi ya Wayahudi.

Kwa sasa, Ye hataruhusiwa kuingia Australia hadi pale atakapowasilisha maombi mapya ya visa ambayo yatafanyiwa tathmini ya kina.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags