Konde Gang yampiga stop Ibraah

Konde Gang yampiga stop Ibraah

Lebo ya Konde Gang Music Worldwide inayomilikiwa na msanii Harmonize imemsimamisha mwanamuziki wake Ibrahim Abdallah, kutoa na kushiriki katika shughuli zozote za muziki hadi suala lake la kujitoa kwenye lebo hiyo litakapopatiwa ufumbuzi.

Hayo yamebainishwa na uongozi wa lebo hiyo kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Mei 11,2025. 

"Uongozi wa kampuni ya Harmonize Entertainment Ltd kupitia lebo yake ya Konde Gang Music Worldwide unapenda kutoa tarifa kwa umma kama ifuatavyo. Mnamo tarehe 03/05/2025, tulipokea barua ya madai (Demand Notice) kutoka kwa Wakili wa msanii wetu, Ibrahim Abdallah Nampunga IBRAAH.

"Barua hiyo iliainisha madai kadhaa ambayo uongozi umeanza kuyafanyia kazi mara tu baada ya kuipokea, kwa mujibu wa taratibu za kisheria na kimkataba. Licha ya juhudi zetu kujaribu kumuelekeza msanii taratibu za kufuata kulingana na mkataba wake. Hivi karibuni, tumebaini kuwepo kwa machapisho, matamshi, na mawasiliano kutoka kwa Ibraah katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii, ikiwemo Instagram na Facebook,"

Taarifa hiyo imeeleza kuwa machapisho hayo yanaonyesha malalamiko na lugha isiyofaa kwa afya ya Lebo pamoja na kumuhusisha mkurungezi muwekezaji wa lebo ambaye bado anaendelea kufanya kazi chini ya Lebo hiyo.

"Tungependa kufafanua kuwa machapisho na matamshi hayo siyo tu yanachafua taswira ya Lebo na wasanii wake, bali pia yanakiuka utamaduni wetu kama Watanzania na kukiuka masharti ya mkataba aliosaini na Lebo hii. Aidha, yanaenda kinyume na sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

"Kampuni yetu inahifadhi haki zake zote za kisheria katika suala hili. Wakati huu ambapo mchakato wa kushughulikia masuala haya unaendelea, umma unapaswa kufahamu kwamba Ibrah bado ni msanii halali wa Lebo ya Konde Gang Music Worldwide na ina haki ya kuendelea au kusitisha mkataba wake kwa kufuata na kuzingatia taratibu rasmi zilizowekwa katika mkataba aliosaini," imeeleza taarifa hiyo na kuongezea kuwa 

"Konde Gang inampiga marufuku Ibraah dhidi ya kuchapisha, kutamka, au kufanya mawasiliano yoyote kuhusu suala hili kwenye vyombo vya habari au mitandao ya kijamii (kama vile Instagram, WhatsApp, Facebook, n.k.). Hii ni pamoja na mawasiliano ya aina yoyote ambayo yanaweza kuharibu taswira ya Lebo au kumdhalilisha mkurugenzi muwekezaji wa lebo ambaye ni msanii,"

Aitha taarifa hiyo imesisitiza kuwa inatoa onyo kali kwamba iwapo masharti hayo  yatakiukwa, Lebo haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi yake katika Mahakama za Tanzania.

Utakumbuka hayo yote yamejiri ikiwa zimepita siku chache tangu msanii Ibraah kuweka wazi kuwa anahitaji kutoka katika lebo hiyo, lakini inamuwia ugumu kutokana na kudaiwa fidia ya Sh1 bilioni






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Christina Lucas


Latest Post

Latest Tags