Kesi ya mtoto wa Diddy yafufuliwa upya

Kesi ya mtoto wa Diddy yafufuliwa upya

Kesi iliyokuwa ikimkabili mtoto wa mkali wa Hip-Hop kutoka Marekani Diddy, Christian Combs ya unyanyasaji wa kingono imerudishwa tena mahakamani ambapo mapema wiki hii kijana huyo alipokea nyaraka za kisheria kutoka mahakamani.

Kwa mujibu wa tovuti ya ‘In Touch’ nyaraka hizo ziliwasilishwa nyumbani kwa Diddy, Miami ambapo kijana huyo anaishi na ndugu zake wengine.

Utakumbuka kuwa wakati wa kesi za Diddy kushamiri na kushika vichwa vya habari duniani kote, naye mwanadada aliyefahamika kwa jina la Grace O’Marcaigh alimshitaki Christian kwa kumshambulia kingono na kumuwekea madawa ya kulevya kwenye kinywaji. Tukio ambalo lilitokea kwenye Yacht ya Diddy mwaka 2022 huku akidai kuwa tukio hilo lilimsababishia mfadhaiko wa kihisia.

Hata hivyo baada ya tuhuma hizo wakili wa Christian, Aaron Dyer hapo awali alijibu kwa kupinga kuwa madai hayo ni ya uongo.

“Haya ni madai mengine ya uongo na yasiyo na msingi sawa na yale aliyowasilisha kwenye kesi ya Rodney Jones,"alisema






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags