Hatimaye Jarida maarufu duniani la Billboard limekamilisha orodha ya wasanii bora 50 na kumtaja Beyonce kama msanii namba 1 wa karne ya 21.
Licha ya kuwa Taylor Swift ni kinara wa mauzo kutoka kwenye album zake, Streams na ziara za muziki ambazo amekuwa akifanya lakini Billboard imetaja Beyonce kutokana na ushawishi pamoja na mchango wake katika miaka yake 25 ya muziki hususa kwenye Pop Music.
Billboard imetoa orodha hiyo kwa kuwajumuisha wasanii ambao wametambulika zaidi ya miaka 25 kwenye muziki huo wa Pop huku Beyonce anashikilia nafasi hiyo ya kwanza huku akifatiwa na Tylor Swift ambaye yupo nafasi ya pili, Rihanna ambaye ameshika nafasi ya tatu, Drake akiwa nafasi ya nne nafasi ya tano ni Lady Gaga,
Wasanii wengine wa Pop ambao wametokea kwenye orodha hiyo ni pamoja na Justin Bieber, Ariana Grande, Adele pamoja na Usher Raymond.
Leave a Reply