Baada ya Billboard kumtangaza Beyonce kama msanii wa kwanza wa Pop wa karne ya 21, Baba yake mzazi mzee Methew Knowles ameibuka na kumpongeza binti yake kwa hatua hiyo kubwa
Mathew Knowles baba wa Beyonce ambae anaaminika ameshiriki mchoro wa mafanikio hayo, amempongeza binti yake pamoja na kumpa ujumbe mtamu unaoangazia mafanikio ya Beyonce.
"Beyoncé alikuwa na aibu alipokuwa mdogo lakini mara tu alipoanza kuimba, ilikuwa kama mtu tofauti aliibuka na tulijua tokea utotoni sana kwamba alikusudiwa kufuata mapenzi yake katika muziki.
"Aligeuza kila mtu ambaye yupo karibu naye na kuanza kumshabikia kitu ambacho kilijengwa kwa bidii yake, maadili ya kazi, uwepo wa majukwaa na kipaji chake" Knowles aliandika kupitia mtandao wa X
Leave a Reply