By Rhobi Chacha
Msanii Ibraah ameondoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na kusema wamezungumzia migogoro iliyopo kati yake na boss wake Harmonize.
Ibraah amezungumza na waandishi wa habari amesema, anashukuru mambo yanaenda vizuri na kila kitu amewaachia uongozi wa BASATA watatoa majibu.
"Nashukuru Mungu mambo yanaenda vizuri, na sababu ya kuitwa ni kuzungumzia migogoro inayoendelea. Kwahiyo tumefanya mazungumzo na BASATA tumewaachia uongozi washughulikie wao watatoa majibu," amesema Ibraah.
Naye Mwanasheria wa Ibraah amesema, BASATA watakapotoa majibu juu ya kinachoendelea Ibraah ataendelea kufanya kazi zake kama kawaida.
"Kuhusu Ibraah kuendelea kufanya kazi zake kama kawaida, tunasubiri majibu ya BASATA,baada ya hapo Ibraah ataendelea na kazi zake kama kawaida," amesema mwanasheria wake Ibraah bila ya kutaja jina lake.
Hata hivyo Harmonize bado hajafika kwenye ofisi hizo, ambazo walitakiwa kufika tangu saa 7 mchana

Leave a Reply