Wondermind Ya Gomez Mbioni Kufilisika

Wondermind Ya Gomez Mbioni Kufilisika

Kampuni ya kusaidia matatizo ya Afya ya Akili iliyoanzishwa na mwanamuziki na mwigizaji Selena Gomez mbioni kufilisika, hii ni baada ya kuondoa wafanyakazi tisa mapema wiki hii kutokana na matatizo ya kifedha.

Kwa mujibu wa Forbes, wafanyakazi kadhaa wa Wondermind waliweka wazi kuwa kampuni hiyo haijawalipa mshahara wao kwa wiki kadhaa lakini pia wanadaiwa maelfu ya dola na wafanyakazi wa kujitegemea (freelancers) pamoja na wasambazaji.

Inaelezwa kuwa Jumatatu Mei 12,2025, wafanyakazi wote wa Wondermind isipokuwa wanne waliitwa mtu mmoja mmoja ambako waliambiwa kuwa wameachishwa kazi, kwa mujibu wa chanzo kimoja kilichoomba jina lake lisitajwe.

Chanzo hicho kilifunguka kuwa taasisi hiyo tayari imeshawalipa wafanyakazi mishahara ya mwezi mmoja waliokuwa hawajalipwa, lakini bado haijatatua suala la mshahara wa mwezi wa pili.

Hata hivyo msemaji wa Wondermind alikanusha taarifa hizo huku akiweka wazi kuwa hana maoni kuhusu chochote cha wafanyakazi kuachishwa kazi lakini tayari wameshasuluhisha tatizo la kifedha linaloikumba kampuni hiyo.


Aidha tukio hilo limeibua mijadala katika mitandao ya kijamii huku wadau na mashabiki wakiuliza maswali katika mitandao ya kijamii kama ni kweli bilionea anaweza kupitia changamoto ya kifedha kwenye kampuni yake.

Utakumbuka Septemba mwaka jana, utajiri wa Selena Gomez uliongezeka na kufikisha dola bilioni 1, huku kwa mujibu wa ‘Bloomberg Billionaires Index’, utajiri wake kwa sasa unakadiriwa kuwa dola bilioni 1.3.

Wondermind ilianzishwa mwaka 2021 na Selena Gomez, mama yake Mandy Teefey, pamoja na mtaalamu wa masuala ya vyombo vya habari Daniella Pierson. Lengo la kampuni hio ni kukuza uelewa na kutoa rasilimali kuhusu afya ya akili kwa njia ya kidijitali na maudhui yanayohamasisha.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags