Ikiwa leo siku ya kwanza ya mfungo wa mwezi Mtukufu wa Ramadhan staa wa muziki Harmonize ametumia mwezi huu wa toba kuwaomba msamaha watu wote aliopishana nao kwa namna moja ama nyingine akiwemo aliyekuwa boss Diamond Platnumz.
Kupitia chapisho lake refu, msanii Harmonize ameomba msamaha akidai kuwa hakuna mkamilifu na alichelewa kutambua makosa yake.
"Safari yangu ya Zanzibar imenivutia bila shaka imekuwa kama ukumbusho kwangu kwamba maisha ya upendo ni bora zaidi kinamna yeyote ile. Sikutakiwa kurushiana maneno na my brother Nasseb samahani sana kaka yangu naomba radhi nilichelewa kutambua hakuna mkamilifu tuliyo fanya pamoja ni mazuri na mengi kuliko shetani alieye kati yetu sioni haja na faida yake," ameandika Harmonize.
Hata hivyo, Harmonize amefichua kuwa mwaka 2018 Diamond Platnumz alimpatia pesa kwa ajili ya kujenga msikiti kijijini kwao lakini kutokana na tofauti zao ujenzi ulisimama kwa kwa muda. Lakini kwa sasa tayari ameshamalizia pesa za ujenzi huo na amependeza uitwe jina la Boss wake wazamani 'Naseeb'.
Utakumbuka kuwa, maelewano mabaya kati ya Harmonize na Diamond yalianza mwaka 2019 baada ya Harmonize kujitoa kwenye lebo ya WCB Wasafi na kulipia zaidi ya Sh 600 milion.

Leave a Reply