Fahamu jina bluetooth limetokana na mfalme mwenye jino bovu

Fahamu jina bluetooth limetokana na mfalme mwenye jino bovu

Inafahamika kuwa katika ulimwengu wa sasa mawasiliano yamekuwa kitu kirahisi sana, yaani ni rahisi kumtumia mtu picha,ujumbe, wimbo, video, document na vitu vingine kwa njia rahisi.

Hayo yote yamewezeshwa na ulimwengu wa teknolojia ambayo ndani yake kuna vitu kama vile kumuhamishia mtu kwa njia ya mtandao bila kutumia ‘waya’, upande huohuo teknolojia hizo zimekuwa zikitajwa majina yake na watumiaji bila kufahamu nini hasa chimbuko la majina hayo.

Kama ulikuwa unatumia Bluetooth bila kufahamu kuhusiana na asili ya neno hilo lilipotokea, basi fahamu kuwa Bluetooth ni jina la mtu ambaye alikuwa mfalme Denmark na Norway.

Kwa mujibu wa historia inaelezwa kuwa mfalme huyo jina lake halisi lilikuwa Harald Gormsson, na jina lake la utani lilikuwa Bluetooth, lilitokana na jino lake moja bovu lililokuwa limeweka rangi ya buluu inayoenda kwenye weusi (Dark blue) na kijivu ndiyo maana wakawa wanamtania Bluetooth.

Hivyo basi mfame huyo alisifika sana kwa kuunganisha watu wa imani na makabila tofauti kuwa na upendo pamoja na mataifa kama vile Denmark na Norway kuwa chini ya utawala wake.

Kutokana na teknolojia ya wireless makampuni mbalimbali ikiwemo ya Ericsson yalichukua uamuzi wa kuungana ili kuwa na njia moja ya mawasiliano ambayo watu wote wangeweza kutumia bila ya uwepo wa ‘waya’.

 Iliwabidi wawakilishi kutoka kila kampuni ya teknolojia ambayo ilikuwaimeungana kufika kwenye mkutano  kuangalia namna na jina gani wangeweza kulitumia katika teknolijia hiyo, ndiyo jina la Bluetooth liliweza kupita, kutokana na sifa za mfalme huyo kufanana na kile wanachotaka kufanya kuunganisha watu kiteknolojia. Bluetooth ilitambulishwa rasmi mwaka 1998






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Asha Charles


Latest Post