Elon Musk adai kuwa Apple imetishia kuiondoa Twitter katika program zake

Elon Musk adai kuwa Apple imetishia kuiondoa Twitter katika program zake

Mmiliki mpya wa kampuni ya mtandao wa kijamii wa Twitter, Elon Musk amedai kampuni ya Apple imeshasitisha matangazo yake mengi kwenye mtandao wa Twitter na kutishia kuiondoka katika program zake bila kutoa sababu.

Inadaiwa kuwa tayari kampuni nyingi zimesitisha matumizi ya Twitter kutokana na mipango ya Musk katika kudhibiti maudhui kwenye mtandao huo.

Apple haijatoa majibu kutokana na shutuma hizo za Musk ambaye anakiri mapato ya Twitter kushuka kwa kiwango kikubwa huku akilaumu wanaharakati kwa madai wanawashinikiza watangazaji wajiondoe.

 






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post