Bifu la wanamuziki kutoka nchini Nigeria waliowahi kutamba na ngoma kama ‘Testimony’, ‘Do Me’, ‘Forever’ na nyinginezo Peter na Paul maarufu ‘P-Square’ linadaiwa kuwakosesha mchongo wa kutumbuiza katika tuzo za Grammy za mwaka huu.
Kufuatia na taarifa iliyotolewa na kaka wa marehemu mfalme wa Pop Marekani Michael Jackson, Jermaine Jackson imeeleza kuwa familia yake iliwapatia dau la pesa wasanii hao waweze kutumbuiza Grammy lakini walikataa.
“Kama sehemu ya kuwashukuru P-Square kwa kuipa thamani staili ya MJ Tribute Dance, tuliwapa ofa ya dola 4 milioni (ikiwa ni zaidi ya Sh 10 bilioni) ili watumbuize kwenye tuzo za Grammys mwaka huu, lakini walikataa.
Familia nzima ya Jackson ilivutiwa sana na heshima ambayo P-Square walimpa Michael Jackson kwenye wimbo wao maarufu ‘Personally’. Si kila siku bendi ya ajabu kama P-Square inakuja. Nilipoona jinsi walivyocheza, nilishangazwa sana kwa sababu ilikuwa ni yakuvutia sana,” amesema kaka wa MJ, Jermaine Jackson
Utakumbuka mwanzoni mwa mwezi Agosti 2024 Paul Nonso Okoye ‘Rudeboy’ alithibitisha kusambaratika kwa kundi la PSquare kwa mara nyingine kwa kudai kuwa toka walivyoungana hakuna cha maana kilichowahi kufanyika.
Kundi la P-Square lilisambaratika kwa mara ya kwanza mwaka 2016 na kuungana tena mwaka 2021, huku mwishoni mwa mwaka juzi kukiwa na tetesi kuwa wawili hao wamegawanyika tena.
Leave a Reply