Bamia inavyoondoa Chunusi Usoni

Bamia inavyoondoa Chunusi Usoni

Mambo vipi mtu wangu wa nguvu, hope huko poua na unaendelea vema na masomo yako hapo chuoni.

Basi leo katika fashion tutaangalia juu ya mboga aina ya bamia jinsi inavyotibu chunusi na kuziondoa moja kwa moja usoni.

Mboga hii mbali na kuondoa chunusi usoni, pia husababisha ngozi kuteleza na kuwa nyororo.

JINSI YA KUFANYA

Chukua bamia zikatekate vipande, ziweke kwenye brenda kisha chukua limao kipande na maji kidogo, weka kwenye brenda kisha saga. Baada ya kupata mchanganyiko wako upake usoni mpaka kwenye shingo, acha kwa muda ikauke kisha bandua kama unavyoondoa maski nyingine usoni.

Fanya hivyo kwa siku tatu kwa wiki itakusaidia kuondoa kabisa chunusi usoni.

Aidha bamia zina uwezo wa kuondoa bakteria usoni na muwasho wa aina yoyote kwenye ngozi. Kama utatumia kwa muda huo utakuwa na ngozi nzuri.

Ila Kumbuka: Usitumie tiba hii kama una tatizo la ngozi au kama una vidonda vyovyote usoni kwani itakusababishia matatizo makubwa.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm


Latest Post

Latest Tags