Amber Rose Amkingia Kifua Diddy

Amber Rose Amkingia Kifua Diddy

Amber Rose, mwanamitindo na msanii amemkingia kifua rapa Diddy Combs akidai kuwa tangu aanze kwenda kwenye party za msanii huyo hajawahi kuona unyanyasaji wa kingono.

Kwenye mahojiano na ‘Club Shay Shay’ Amber amefunguka kuwa hajawahi kuona matendo mabaya katika White Party hizo huku akisisitiza kuwa Diddy alikuwa muda wote akizungumza na wasanii wenzake.

“Nimehudhuria kila sherehe za Puff. Nimekuwa kwenye kila White Party tangu 2009, sijawahi kushuhudia unyanyasaji wowote ule, Kila mara nilipokuwa pale, Puff alikuwa pale muda wote,” amesema Amber

Aidha mbali na hilo amefunguka kuwa hajawahi kuona ushahidi wa moja kwa moja wa madai hayo, lakini alikubali kuwa tuhuma za unyanyasaji dhidi Cassie zipo. "Alimnyanyasa Cassie, sote tumeona video hiyo."

Utakumbuka Sean "Diddy" Combs anakabiliwa na mashtaka kadhaa katika mahakama ya shirikisho nchini Marekani. Mwezi Septemba 2024, alishtakiwa kwa makosa yanayohusiana na ulanguzi wa ngono kwa nguvu, usafirishaji kwa ajili ya ukahaba, na kula njama za ulaghai.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Aisha Lungato

A digital journalist and writer for Mwananchi Scoop. My stories are around entertainment, lifestyle, artist profiles and career.


Latest Post

Latest Tags