Offset Apuuzia Msimamo Wa Lebo Yake

Offset Apuuzia Msimamo Wa Lebo Yake

Rapa Offset amepanga kutumbuiza katika tamasha litakalo fanyika Moscow, nchini Urusi licha ya lebo inayomsimamia Universal Music kusitisha kufanya shughuli za muziki nchini humo.

Mwanachama huyo wa zamani wa ‘Migos’ ambao walitamba na ngoma kama Bad and Bouje, ametumia ukurasa wake wa Instagram kufichua habari hizo ikiwa ni baada ya kumaliza ziara yake ya muziki nchini Marekani.

Rapa huyo ambaye amesainiwa chini ya lebo ya 'Motown Records' inayomilikiwa na Universal Music Group kampuni mama ambayo hapo awali ilitangaza kutofanya shughuli zake Urusi baada ya uvamizi wa Ukraine 2022.

"Tunahimiza kukomeshwa kwa machafuko nchini Ukraine haraka iwezekanavyo, Tunazingatia vikwazo vya kimataifa na, pamoja na wafanyakazi wetu na wasanii, tumekuwa tukifanya kazi na makundi kutoka mataifa mbalimbali ili kuunga mkono juhudi za misaada ya kibinadamu kuleta msaada wa haraka kwa wakimbizi katika eneo hilo." ilisema taarifa ya UMG

Hata hivyo, Dababy ni rapa mwingine ambaye amesainiwa na lebo ambayo ipo chini ya mwamvuli wa Universal Music, pia alitumbuiza nchini Urusi hivi karibuni.

Aidha, Offset ambaye alikuwa mume wa rapa Card B kabla ya kutengana mwaka 2024 anaendelea kupata changamoto za kisheria ikiwa ni pamoja na wizi na umiliki wa silaha bila kibali.

Tangazo la Offset kutumbuiza nchini Urusi linakuja baada ya kuvuma kwa habari kuwa Ikulu ya White House, Marekani inaelekea kuondoa vikwazo dhidi ya Urusi.






Comments 0


Leave a Reply

Author

Hello, I'm
Masoud Kofii


Latest Post

Latest Tags