Tovuti ya Billboard imetangaza wimbo wa 'Blinding Lights' kutoka kwa The Weeknd umekuwa wimbo bora kwenye orodha ya Nyimbo 100 Bora za Karne ya 21.
Blindin Light ambao ulitoka Novemba 29, 2019 ulivunja rekodi ya kukaa wiki 57 mfululizo kwenye nyimbo 10 bora za chati ya Hot 100, ikiwa na wiki nne kwenye nafasi ya kwanza, na wiki 86 kwenye orodha ya nyimbo 40 za juu ya chart hiyo.
Mwaka 2021, wimbo huo ulichukua pia taji la Billboard's Greatest of All Time Hot 100 Songs huku The Weeknd akitoa shukrani kwa mashabiki wanaomsapoti.
Hata hivyo Januari 9, 2025 Chati hiyo kubwa ya muziki Duniani ilimtaja The Weekend kama msanii namba 6 kwenye orodha ya wasanii 100 bora na waliofanya vizuri kwenye chati hiyo kwa karne ya 21, kuanzia miaka ya 2000 mpaka 2024.
Leave a Reply